Utangazaji

Ikiwa unanuia kuanzisha idhaa ya TV ya mtandaoni, redio ya ndani ya duka au upeperushaji tukio moja kwa moja, tunaweza kukusaidia.

Tukiwa na timu kubwa ya wanahabari wa kutangaza na wafanyakazi wa utayarishaji, tuko katika nafasi nzuri ya kutoa huduma bora, haijalishi ukubwa wala udogo wa hitaji la tangazo.

Tunaweza kutayarisha tangazo la haraka la dakika tatu la redio au TV kwa gharama nafuu, utoaji maoni mkamilifu kuhusu matukio mbalimbali ya michezo na matangazo makubwa zaidi yanayohusu utumiaji wa mwangaza, nje ya vyombo vya utangazaji (utangazaji wa nje ya studio) na utayarishaji wa jukwaa kwa usaidizi wa mtaalamu na washirika wetu wa kuaminika.