Maoni na Matangazo

ICS ni wataalamu wa kutoa maoni na matangazo, haswa kuhusu matukio ya michezo.

Tunaweza kufanya haya kwa njia ya kipekee kama utoaji maoni studioni ambapo watangazaji wetu wanatumia picha kama chanzo cha habari ili kukupa sauti halisi. Pia tunaweza kushirikiana na wamiliki wa haki kupeperusha na kufanya mipasho rasmi kuwa biashara.

Kwa wapokeaji fedha za bahati nasibu, utoaji maoni ni muhimu kwa kuboresha hali ya kuweka dau na kuhimiza zaidi katika uwekaji dau, huku pia ikitoa huduma za simu na programu maarufu za redio.

Tunatoa maoni huru kwenye mechi zote kutoka Ligi ya Uingereza, Mashindano ya Ubingwa wa Vilabu vya Ulaya na ligi nyingine za kandanda za Ulaya na pia mashindano makuu ya soka ya kimataifa. Pia sisi ni wasambazaji rasmi wa utoaji maoni ya mbizo za farasi Uingereza, ambayo tunaweza kutoa kwa lugha yoyote inayohitajika kupitia ushirikiano wetu na GBI na tunatoa maoni kuhusu matukio makuu ya michezo kama vile Kombe la Dunia la Raga na pia mchezo wa Kriketi ya Majivu (Ashes Cricket).

Pia tunatoa maoni ya maandishi ya kila dakika ambayo ni ya kujuza na kuburudisha kutokana na mtindo wake wa mtiririko na shirikishi. Huku yakiwa na wastani wa taarifa 60 kwa kila mchezo, matukio yote muhimu kama vile mabao, kadi nyekundu, kadi za njano na mabadiliko yanajumuishwa. Pia tunaangazia vipengele vingine muhimu vya mchezo, pamoja na mbinu, umahiri, vipindi vya mchezo mzuri na mbaya na maamuzi makubwa ya marefarii.

Wakati huo huo, kipindi chetu cha kuvutia cha redio Football Live hukuletea taarifa za mabao za moja kwa moja, maonyesho ya awali ya mechi na kuripoti kutoka ligi zote kuu za Ulaya kila Jumamosi na Jumapili alasiri.