Video

ICS huangazia utayarishaji wa video za haraka na zinazovutia za gharama nafuu, jambo ambalo huwaruhusu wateja kuwapa watazamaji wao matangazo ya teknolojia ya hali ya juu.

Video ni njia imara ya uhusishaji na inashirikiwa kwa urahisi kwenye mitandao ya jamii. Inaweza kuboresha kurasa za maudhui zinapopachikwa, wakati wa kuunda idhaa ya YouTube iliyo na orodha ya kucheza ya maudhui yanayofaa, inaweza kumnufaisha mteja kwa njia nyingi.

Tunawaajiri maripota maalum ambao ni wasomaji habari na watangazaji wenye ujuzi na wanaweza kuangazia mada yoyote inayovuma au tukio lijalo.

Kwa mfano, waleta habari wetu wanaweza kutoa maonyesho ya awali ya video zinazoburudisha na uchanganuzi wa mpira wa miguuwa wikendi, mbio za farasi aumatukio mengine ya kuweka dau ambayo yanaweza kuboreshwa anavyotaka mteja. Watangazaji wetu watalaamu wanaweza pia kuhusisha mazungumzo yao na matumaini na matangazo ya mpokea fedha za bahati nasibu ili kuimarisha uhamasishji.

ICS pia inaweza kuunda video za kipekee za utafutaji soko kuhusu mada mbalimbali, kazi iwe kubwa au ndogo. Mbali na videoza maonyesho ya awali ya michezo, tuna tajiriba ya kuongoza na kufanya maudhui yavutie kuhusu mada kama vile watu mashuhuri, burudani na siasa.