Uwezo wa Kupata Soko

Utafutaji soko wa mshirika unaweza kuwa njia nafuu na yenye tija zaidi ya kuwavutia wateja wapya kwenye biashara yako.

Tuna timu ya ndani ya watafutaji soko wenye ujuzi na tajiriba ambao wanaweza kudhibiti na kukuza washirika wako waliopo na pia kuanzisha mipango mipya ya washirika.

Timu yetu yenye wataalamu inaangazia kuajiri na kusimamia washirika na ina uwezo wa kufikia tovuti nyingi za washirika watarajiwa, kukusaidia kuanzisha na kuongeza idadi ya washirika wako.

Hapa ICS, tunaweza kuzifanya huduma zetu zifae mahitaji yako na tutasimamia kampeni zako za washirika kwa jumla au kiasi, kutegemea mahitaji yako. Tunaweza kufanya haya kwa lugha mbalimbali na pia kwenye mataifa kadhaa.

Sisi ni wataalamu wa tasnia mbalimbali, ikiwemo michezo, bima, fedha, mawasiliano ya simu, utalii, spoti na biashara rejareja. Tunaweza kushughulikia miradi ya muda mfupi na ya muda mrefu, pamoja na matokeo dhahiri ya huduma ya mradi na kwa gharama nafuu wakati wote.

Tumeshughulikia kwa ufanisi kampeni za muda mrefu za wateja wa kuaminika na kwa uhusiano wetu imara, maarifa ya tasnia ya washirika na miundombinu inayoweza kukua;tunaweza kutoa huduma thabiti za utafutaji soko la washirika inayoweza kuboreshwa kwa ajili ya mahitaji ya wateja binafsi.